Mapitio ya washirika walioko katika ngazi moja: Tazama wengine wanavyofanya!
Hakuna mbinu zinazofanana zinazoweza kutumika kwa msaada wa washirika na michakato ya mapitio. Mitandao ya kitaifa ya Kongani la Kimataifa na mashirika yanayowezesha yanapaswa kubadilika na kufanya majaribio ya kile kinachofaa zaidi kwao. Uzoefu husika upo, miongoni mwa mengine, katika Ufilipino, Ekuador, Kolombia, Indonesia, na Uchina. Tazama hapa chini kwa habari zaidi kuhusu msaada na michakato ya mapitio kwa washirika walioko katika ngazi moja nchini Iran na Uhispania.
Mchakato wa kusaidia na mapitio ya washirika walio katika ngazi moja nchini Iran
Mchakato wa hatua nne umeainishwa na Muungano wa Makabila ya Wahamaji asilia ya Iran, kwa kushirikiana na Cenesta, ambacho ni Kituo cha Maendeleo Endelevu na Mazingira.
- Katika hatua ya kwanza, jamii zenyewe zinafanya tathmini tatu:
1) tathmini ya eneo, inayohusisha uchoraji ramani shirikishi wa eneo lao la jadi;
2) tathmini ya ikolojia, inayohusisha kuongeza rasilimali za ikolojia kwenye ramani, mwelekeo wa sasa wa ikolojia na maarifa yote asilia wanayoona yanafaa; na
3) tathmini ya utawala, inayohusisha kutambua taasisi ya utawala wa kimila na-ikiwa muhimu – hatua za kuuimarisha.
- Katika hatua ya pili ikiwa matokeo ya tathmini tatu yatadhihirisha kuwa eneo hilo linaweza kuchukuliwa kuwa eneo la hifadhi ya jadi la Kongani la Kimataifa—, basi jamii inachukua uamuzi huru na wa hiari wa kujitambua; kisha kutuma kumbukumbu zake za eneo la hifadhi ya jadi kwa Muungano wa Makabila ya Wahamaji asilia ya Iran kwa maoni zaidi na maswali.
- Katika hatua ya tatu, maoni na maswali yote yanapotatuliwa, Muungano wa Makabila ya Wahamaji asilia ya Iran huwasilishakumbukumbu na taarifa yoyote ya ziada kwa Masijala ya Kitaifa ya Kongani la Kimataifas nchini Iran, ambayo inatunzwa na Cenesta.
- Katika hatua ya nne na ya mwisho, Cenesta inatayarisha kumbukumbu ili zijumuishwe katika Masijala ya kimataifa ya Kongani la Kimataifa na/au Kanzidata ya Dunia ya Maeneo Yanayohifadhiwa. Katika hatua hii, taarifa pia hutumwa kwa mashirika husika ya serikali, kwa taarifa na kujumuishwa katika ripoti zao mikataba ya kimataifa.
Ziara ya Cenesta kusaidia hatua ya kwanza ya mchakato wa msaada na mapitio wa washirika walio katika ngazi moja
Mchakato wa msaada na mapitio ya washirika walio katika ngazi moja nchini Uhispania
Mnamo 2015, Iniciativa Comunales iliandaa “Itifaki ya kwanza ya mapitio ya washirika walio katika ngazi moja ya wanaotafuta usajili katika Masijala ya Kongani la Kimataifa nchini Uhispania”. Iniciativa Comunales ni muungano wa jamii za wenyeji ambao kwa pamoja hutawala rasilimali, ikiwakilisha maelfu ya watu wa kawaida nchini Uhispania. Wanachama wengine ni pamoja na mashirika ya kusaidia na watu binafsi wanaoguswa. Mnamo 2017, jamii mbili za kwanza zilisajiliwa katika Masijala ya Kongani la Kimataifa na, kufikia 2020, michakato sita ya usajili ilikamilika na nyingine zaidi kuanzishwa. Toleo la sasa la itifaki liliidhinishwa mnamo 2019 (pakua kwa Kihispania).
Tangu mwanzo, kulikuwa na maafikiano makubwa miongoni mwa jamii kuhusu haja ya kudhamini ubora wa masijala. Ili kuepuka “hadaa”, ilikuwa muhimu kwamba mchakato uhakikishe kuwa maeneo yaliyosajiliwa yalikuwa na sifa tatu za ‘maeneo ya hifadhi ya jadi’: 1) uhusiano imara kati ya jamii na eneo; 2) taasisi ya utawala inayofanya kazi vizuri na 3) matokeo ya uhifadhi wa maliasili na michango kwa kipato cha kujikimu na ustawi.
“Mlinzimwanamke” wa jamii ya wakusanya magamba ya konokono. Picha: iComunales.
Kwanini inahitajika?
Ili kuelewa vyema mashaka ya jamii kuhusu ubora wa masijala, ni muhimu kutaja hilo kuwa nchini Uhispania kuna maeneo mengi yanayotawaliwa na jamii (kwa mfano “kawaida”); hata hivyo, ufanisi wa utawala wa jamii katika baadhi maeneo ni kama haupo kwa sababu ya mmomonyoko wa kitamaduni, uhamaji na idadi kubwa ya watu wazee. Baadhi ya jamii hizi hutia saini makubaliano ambayo watendaji wa nje (kawaida makampuni) husimamia maliasili za eneo hilo kwa ya vigezo vyao vya soko kwa kipindi cha miaka. Hii ina madhara makubwa kwa utawala wa ndani, malengo ya uhifadhi na matumizi mengine ya eneo ya kijamii na kipato cha kujikimu. Kwa mfano, chini ya mikataba hii maeneo makubwa ya kawaida hufanywa kilimo cha aina moja tu kwa kupanda Mikaratusi (Eucalyptus), aina vamizi ya miti ya kigeni – kwa ajili ya kukata miti kibiashara kwa muda mfupi tu. Kwa hivyo, jamii hupoteza nguvu yao ya utawala kila siku, na mtazamo wao hubadilika kutoka kuwa uhusiano mzuri wenye tija wa kitamaduni kwa eneo, hadi kuwa kutafuta mapato tu.
Iwapo kwa hali kama hizi, Masijala itajumuisha kwa uaminifu tu kama maeneo halisi ya jadi, itajumuisha “hadaa” na kupunguza thamani ya Masijala na uwezo wa jamii zilizosajiliwa kuitumia kama chombo cha utetezi. Kwa sababu hii, jamii zilikubali kupokea maoni na maswali kutoka nje kwa wanachama wa jamii nyingine mbili bila majina kwa ajili ya “ripoti ya marekebisho”. Ripoti hizi ni za siri, na uzoefu wetu ni kwamba ukosoaji unaojenga kutoka kwa washirika walio katika ngazi moja unaweza kuwa kichocheo kikubwa cha uimarishaji wa ndani wa michakato ya jamii.
Inafanyaje kazi?
Jamii zinazotuma maombi zinakubali kupitia mchakato shirikishi wa msaada na masahihisho ya washirika walio katika ngazi moja kwa kuzingatia:
• Taarifa zinazotolewa na jamii zilizotuma maombi katika fomu rasmi za Kituo cha Ufuatiliaji wa Uhifadhi Duniani cha Mpango wa Mazingira wa Shirika la Umoja wa Mataifa (shirika linalosimamia Masijala ya Kongani la Kimataifa) na Iniciativa Comunales (shirika wezeshaji).
• Ripoti ya masahihisho kutoka kwa jamii mbili za washirika walio katika ngazi moja ambazo hazifahamiki kwa majina
• Taarifa nyingine yoyote muhimu iliyotolewa na jamii zilizotuma maombi au wengine.
Mchakato huu unawezeshwa na Iniciativa Comunales. Mara taarifa na ripoti za marekebisho zitakapokamilika, Kamati ya Uongozi ya Iniciativa Comunales inaleta kwenye mkuu mkutano wa chama maoni yenye sababu kuhusu waliotuma maombi. Uamuzi wa mwisho basi utachukuliwa na wanachama wote kwa pamoja (kulingana na kanuni za chama, kura za jamii wasio wanachama, ikiwa ni pamoja na watu binafsi, AZAKi, vituo vya utafiti, na kadhalika, haziwezi kuzidi 40% ya jumla).
Itifaki inaongoza mchakato huu; na mahitaji yanapojitokeza, itifaki hupitiwa upya na kurekebishwa. Mabadiliko yaliyopendekezwa hujadiliwa mara kwa mara, ili kuidhinishwa na mkutano. Itifaki pia husimamia marekebisho ya washirika wote walio katika ngazi moja waliosajiliwa na Kongani la Kimataifa kila baada ya miaka mitano.
Tulichojifunza
• Jamii nyingi, ikiwa ni pamoja na waombaji dhahiri, hawaoni kusajiliwa kama fursa nzuri, bali hupelekea kutambuliwa ‘pekee’. Kitu cha zaidi kinahitajika.
• Mchakato wa wazi wa mapitio ya washirika walio katika ngazi moja una changamoto; unahitaji kujitoa kwa nguvu zote kwa wanachama wa Mtandao wa Kongani la Kimataifa (ambayo iko kwa Uhispania), au bajeti kubwa (haipo kwa Uhispania); katika hali zote, inahitaji muda mwingi na uzoefu na watu wanaowajibika. Kuna rejea chache za hapo awali na ni ngumu kupata usawa, kati ya “kuifanya rahisi” na kutengeneza mfumo wa kuaminika unaozingatia mahitaji ya kila mtu anayehusika na kuepuka uchovu wa pamoja. Tuna wasiwasi kuhusu hili na tunachunguza mbinu mpya za kuboresha ustahimilivu wa mchakato.
• Kuna mapungufu makubwa ya “mfumo wa medali” ambao unazingatia tu mifano ya nembo zaidi za maeneo ya hifadhi ya jadi. Hii inaweza kuwa na matokeo potofu ya kukuza usomi. Jibu la sura mbili “ndiyo/hapana” kwa swali “hili ni eneo la hifadhi ya jadi?” haijumuishi matukio mengi, kulingana na picha tuli katika muda fulani, kupuuza juhudi za sasa, michakato au mienendo.
• Kusajiliwa kupitia mbinu hii kuna uwezo mdogo wa kubadilisha. Mbinu mpya, jumuishi inahitajika, ili kutoa utambulisho unaoeleweka na msaada kwa jamii yoyote inayotafuta kujumuishwa katika Masijala – bila kujali sifa yake ya sasa kama Kongani la Kimataifa au la. Tunafanyia kazi mbinu hii hivi sasa, ambayo sisi tunaiita Vivero (“kitalu cha mimea” kwa Kihispania, tazama mchoro hapa chini).
• Utaratibu unapaswa kuwepo ili kujumuisha kutokukubaliana kwa njia inayojenga. Nia njema na “kucheza kwa haki” haipaswi kuchukuliwa kawaida. Afadhali tuchukue kilicho bora zaidi kutokana na kutokubaliana kwa kujenga lakini tuzuie na kupinga nafasi na vitendo vya uharibifu.
• Mfumo wa utawala uliokamilika na wazi unapaswa kuwepo, ikijumuisha bodi inayoaminika kwa ajili ya kutatua migogoro na kuchukua maamuzi ya mwisho, na sera ya kuepusha mgongano wa masilahi. Ili kupunguza kulimbikiza madaraka, bodi hii inapaswa kuwajibika kwa uwakilishi mpana wa jamii ambazo baadaye zitaomba kusajiliwa. Maamuzi yake yanapaswa kuwa ya kuweza kukatiwa “rufaa” na muundo wake kuwa wa kutokana na “mabishano”.
• Washiriki wote wanapaswa kukubali kwa uwazi kufuata kanuni za kawaida zilizowekwa.
• Kukosekana kwa usawa kunapaswa kuangaliwa kwa makini sana katika sifa za kijiografia na za kisekta kwa wanaoomba Usajili kwa sababu zinaweza kusababisha upotoshaji katika uwezo wa uwakilishi: ikiwa mikoa au sekta fulani (kwa mfano, misitu, umwagiliaji, uvuvi) hutawala maoni juu ya nini ni eneo la hifadhi ya jadi na jinsi linavyopaswa kuwa, zingine zinaweza kutengwa. Hapo awali tulishindwa kuliona hili lakini tunajifunza kuboresha.
Mawazo juu ya mbinu ya baadaye ya Masijala ya Kongani la Kimataifa
Tunafanya kazi ili kujenga mchakato wa pamoja ili kusaidia jamii zote zilizo tayari kuimarisha sifa tatu muhimu za maeneo yao ya jadi, bila kujali jinsi kila moja ina nguvu kiasi gani kwa wakati fulani au kama wanavutiwa na Usajili au la. Katika mchakato huu wa msaada, Usajili haupaswi kuwa lengo la muda mfupi, lakini mojawapo ya zana nyingi za kuboresha sifa za Kongani la Kimataifa za eneo fulani kama sehemu ya mbinu ya muda mrefu.
Ili kuelezea mchakato huu tunapendekeza “Vivero de ICCAs”, (“kitalu cha mimea cha Kongani la Kimataifa”): badala ya “uamuzi wa ndiyo au-hapana” (aidha unastahili kutambuliwa au kutupiliwa mbali), umakini utaelekezwa kwa muendelezo wa kiwango cha vizingiti vya changamoto na mafanikio katika kila moja ya sifa tatu, na taratibu na uelekeo ambazo jamii inakuza. Hii pia itakuwa fursa kwa jamii za Kongani la Kimataifa ambazo tayari zimesajiliwa kuonyesha uzoefu wao na kusaidia wengine kuboresha mifumo ya utawala, mikakati ya uhifadhi na mambo mengine, huku wakiendelea kujifunza na kuimarisha maeneo yao ya kadi – kwa maana ya kweli ya “msaada kwa washirika walio katika ngazi moja”
Imetayarishwa na Iniciativa Comunales; kwa habari zaidi, andika kwa: hola@icomunales.org