Tunajua nini tayari? Maswali ya kujadili mashinani.

Kama sehemu ya kujadiliana mashinani, haya maswali yanaweza kusaidia jamii kuanza na kuweka kumbukumbu kwa kubainisha ni nini (na bado) hakijajulikana na kuamua juu ya maeneo ambayo uwekaji kumbukumbu zaidi kunaweza kuwa muhimu. Ni kwamba hakuna uwezekano kuwa maelezo haya yote yatapatikana mwanzoni. Kujadiliana hutumika kupata mawazo kuhusu wapi na jinsi gani ya kupata baadhi ya majibu inaweza kuwa mahali pa kuanzia kuweka kumbukumbu kadiri muda unavyokwenda. (Ona pia #kioleza)

.. vipengele muhimu vya eneo

 • Eneo la hifadhi la jadi liko wapi na linajumuisha maeneo/rasilimali gani?
 • Je, eneo la hifadhi la jadi limekamilika vyema, kwa mfano, lina mipaka iliyo wazi?
 • Je, mipaka hii imebadilika kwa muda? Namna gani na kwa nini?
 • Eneo la eneo la hifadhi ya jadi linalokadiriwa kuwa na ukubwa gani?
  Je, kuna ramani au viwianishi vya Mfumo wa Taarifa za Kijiografia vinavyopatikana?
 • Je, kuna mwingiliano wowote na maeneo ya hifadhi au maeneo mengine yanayotawaliwa na serikali au wahusika wengine?
 • Ni nini hali ya mazingira katika eneo la hifadhi ya jadi (kwa mfano, ubora, unzuri, hatarini, maskini, imeharibiwa kupindukia)?
 • Je, kuna kumbukumbu au taarifa zilizopo za kuthibitisha majibu yetu kwa maswali haya?

Kumbuka: Ingawa inafaa kujua eneo la hifadhi ya jadi liko wapi, mipaka sahihi iliyowekwa na kubainishwa SIYO muhimu.

… jamii ya wamiliki

 • Jamii yetu ya wamiliki iko wapi na kubwa kwa kiasi gani?
 • Je, jamii yetu imekaa kwa kudumu palepape tu au ina hama hama? Ikiwa ina hama hama, tunalo eneo maalum la mifugo inayohama hama?
 • Je! ni lugha gani zinazozungumzwa au kutumiwa na jamii yetu?
 • Je, jamii yetu ni ya aina moja au kuna tofauti kubwa ndani yake kuhusu mamlaka, utajiri, utendaji kazi, dini, lugha, kabila au sifa nyinginezo?
 • Ikiwa ndivyo, je, tofauti hizi zinaonyeshwa katika njia mbalimbali tunazozihusianisha na eneo letu la hifadhi ya jadi?
 • Je, jamii yetu ina utamaduni gani, sherehe za aina gani, taasisi na/au kanuni?
  Ikiwa ndivyo, vipengele hivi vya pekee vinahusiana katika njia zipi kuu na eneo la hifadhi ya jadi?
 • Je, jamii yetu imeendelea vizuri, inastarehe, inatatizika, au ni maskini na iko katika mazingira magumu?
 • Je, jamii yetu ina mshikamano wa ndani wenye nguvu, au kuna migawanyiko mikubwa ya ndani na mivutano?
 • Je, kuna kumbukumbu au taarifa zilizopo za kuthibitisha majibu yetu kwa maswali haya?

… tunu za eneo

 • Jamii yetu hutumia jina mahususi kuzungumzia eneo letu la hifadhi ya jadi? Kama ndio, jina gani?
 • Ni tunu au manufaa gani muhimu ya eneo la hifadhi ya jadi kwa jamii yetu? Kwa mfano, ni chanzo ya chakula, maji, kipato? Je, inatumika kwa mikusanyiko ya sherehe au madhumuni mengine ya kitamaduni au ya kiroho? Je! linahifadhi kumbukumbu au miili ya mababu? Linahifadhi rasilimali kwa nyakati za uhaba au mtikisiko wa kijamii? Linazuia majanga ya mazingira? Linahusiana na utambulisho wa jamii na mtazamo wa ulimwengu? Ni muhimu kuhifadhi bioanuwai (kwa mfano, kuna aina ya wanyama au miti, au utendaji wa mifumo ikolojia ambayo iko vizuri inayojulikana na kuthaminiwa au kulindwa?)
 • Je, eneo la hifadhi ya jadi linafurahiwa na kuthaminiwa kwa usawa ndani ya jamii yetu? Ikiwa sivyo, ni nani anayevutiwa zaidi na kwa nini?
 • Je, eneo la hifadhi ya jadi lina tunu gani (kama zipo) kwa watu wasio wa jamii yetu?
 • Je, kuna kumbukumbu au taarifa zilizopo kuthibitisha majibu yetu kwa maswali haya?

… utawala na usimamizi—njia za kufanya na kuheshimu maamuzi na kujali eneo la hifadhi ya jadi

 • Malengo makuu ya jamii yetu ya kutunza eneo la hifadhi ya jadi ni yapi?
 • Maamuzi makuu kuhusu eneo la hifadhi ya jadi yanafanywaje na yanafanywa na nani?
 • Makundi mbalimbali – yakiwemo ya wanawake na vijana – yanahusika vipi katika kufanya maamuzi haya?
 • Baraza la uongozi (au mabaraza) liliundwa lini na jinsi gani na kwa nini limebadilika?
 • Je, baraza la uongozi (au vyombo) liliundwa na jamii yetu, au na taasisi nyingine, au vyote?
 • Maamuzi gani mahususi – kwa mfano uundaji kanda na mipango na sheria zingine – tumeridhia kwa eneo?
 • Je, maamuzi yetu ni wazi na yanajulikana vyema kwa wote?
 • Ni nani anayesimamia eneo kihalisi na kutekeleza maamuzi yanayochukuliwa na baraza la uongozi?
 • Je, kuna mfumo wa ufuatiliaji wa matokeo ya usimamizi na, kama ni hivyo, nani anahusika na kwa nini?
 • Je, wanajamii wetu hujifunza vipi kuhusu kanuni na kujihusisha na eneo la hifahdi ya jadi?
 • Je, jamii yetu inachukua hatua ili kuhakikisha kwamba wengine wanafahamu na kuheshimu maamuzi na kanuni zetu kuhusu eneo la hifadhi ya jadi (kwa mfano, kanuni za kupata na kuzitumia rasilimali)? Kwa namna gani?
 • Je, haki na majukumu ya jamii yetu ya kudhibiti eneo yanatambuliwa? Ikiwa ndiyo, ni aina gani ya utambulisho (ya kawaida na/au ya kisheria)?
 • Je, kuna kumbukumbu zilizopo au taarifa maalum ya kuthibitisha majibu yetu kwa haya maswali?
 • Kuimarisha eneo lako la hifadhi ya jadi: mwongozo kutoka kwa jamii kwa ajili ya jamii
 • Je, wadau wengine (nje ya eneo la hifadhi ya jadi) wanatambua na kuheshimu haki na wajibu wa jamii na eneo la hifadhi ya jadi kwa vitendo? Je, kuna migogoro mikubwa kuhusu umiliki wa ardhi na/au matumizi ya maliasili?