Kujitambua kama mmiliki wa eneo la hifadhi ya jadi: Maswali ya kujadili mashinani

Timu ya uwezeshaji inaweza kutoa maswali hapa chini ili kusaidia jamii kujiimarisha kujitambua kama mmiliki wa eneo la hifadhi ya jadi. Hili linaweza kufanyika kabla, wakati au baada ya majadiliano ya mashinani yaliyolenga kuendeleza maono/dira ya siku zijazo.

  • Je, ni wazi kwamba baadhi ya chaguo zitakazofanywa leo— na serikali, sekta binafsi, jamii nyinginezo au sisi wenyewe- zitaathiri kwa kiasi kikubwa mustakabali wa eneo letu la hifadhi ya jadi na sisi wenyewe? Je, tuna mfano wowote wa hizo chaguo?
  • Je, kuna baadhi ya maamuzi ya kimsingi ambayo jamii inaweza kufanya leo kuathiri chaguo kama hizo? Je, sisi tuna mfano wowote wa maamuzi kama hayo?
  • Je, tunaweza kujiwazia katika siku zijazo kama jamii inayostawi inayofanya kazi kama mmiliki wa eneo la hifadhi ya jadi linalostawi? Je, tunaweza kuwa tunaishi vizuri, tukifanya kazi na kutegemeza vipato vyetu vya kujikimu huku tukidumisha eneo letu la hifadhi ya jadi katika hali ya kustawi?
  • Je, hilo linaweza kumaanisha nini kwa jinsi tunavyoishi, kufanya kazi na kujipanga? Je, tuko tayari na tuna hiari kufanya hivi?
  • Je, tuko tayari kujitoa kuunga mkono chaguo kama hizo, kwa mfano kutia saini ahadi, ya mkataba au orodha ya kanuni na vigezo ambavyo tuko tayari kufuata katika uhusiano wetu na eneo la hifadhi ya jadi?
Note

Njia bora ya kusaidia jamii yako kuona mustakabali wake wa baadaye na kuchukua maamuzi muhimu kuhusu hilo ni kuwasafirisha baadhi ya wawakilishi kuona nini kimetokea katika maeneo mengine kutokana na chaguo na maamuzi yaliyofanywa na jamii nyingine, serikali na wengine. Wawakilishi wako watakaporudi, watashiriki kile walichojifunza, kuwajulisha wengine na kufafanua uwezekano wa matokeo ya matendo yako.