Tafakari

Michakato ya kujiimarisha inaweza kuchochewa na hitaji la kushughulikia suala kubwa la eneo lako au kuchukua fursa mpya. Katika hali zote, sehemu muhimu ya kuanzia ni kufanya majadiliano kuanzia mashinani/chini ili kuchunguza na uthibitishe:

  • kama jamii yako ni mmilikiwa hifadhi wa eneo la hifadhi ya jadi;
  • hali ya eneo hilo la hifadhi ya jadi ikoje; na
  • Ni kwa jinsi gani jamii yako inataka kuingia kwenye mchakato wa kujiimarisha yenyewe.

‘Maeneo ya hifadi za jadi ni tofauti tofauti sana… lakini maeneo ya hifadhi ya jadi ‘yaliyokamika vyema’ yana sifa tatu zinazofanana:

  • Kuna ukaribu na uhusiano mkubwa wa hali ya juu kati ya eneo na wamilik wa jadi au watu wanaoishi eneo hilo,
  • Wamiliki au jamii husikajamii wanaweza kufanya na kutekeleza maamuzi na sheria (kwa mfano kuhusu kupata na kutumia) kuhusu eneo. Yaani kuwa na mfumo wa utawala bora
  • Maamuzi ya kiutawala na juhudi za usimamizi za wamiliki au watu wa jamii husika huchangia katika kuhifadhi eneo na kuhakikisha kipato cha kujikimu na ustawi wa jamii husika.

Inasaidia kuelewa ‘hali’ ya eneo lolote la jadi lililopo au linalowezekana kuwepo, yaani, iwe ni eneo:

  • lililokamilika—eneo kwa sasa lina sifa zote tatu, yaani, muunganiko/mahusiano ya kina kati ya eneo na jamii, mfumi wa utawala bora wa jamii, na matokeo bora ya uhifadhi na riziki/ustawi;
  • lililoharibika — eneo lilikuwa na sifa zote tatu, lakini kwa sasa baadhi hazipo kikamilifu kwa sababu ya misukosuko ambayo jamii ya wamilikiwamiliki/waangalizi inaamini kuwa inaweza kubadilishwa na kuwa kama ilivyokuwa awali au kubadilishwa; au
  • linalotarajiwa — eneo halijawahi kuwa na sifa zote tatu, lakini lina uwezo wa kuzianzisha; kulingana na jamii ambayo iko tayari kuwa mmiliki wake.

Bila kujali hali ya eneo la hifadhi ya jadi, mchakato wa kujiimarisha wenyewe unaweza kuisaidia jamii ya wamilikiwamiliki kuielewa na kuitunza vyema. Jamii hukamilisha na kuuongoza mchakato wa kujiimarisha yenyewe. Hili linahitaji kujitoa na (mnyumbuliko) mpango. 

Note

Kumbuka: Kwa mwongozo huu wa mtandaoni, ‘jamii’ ni neno la jumla linalotumiwa kumaanisha wanaojitambulisha kama wamiliki na wamiliki wa eneo fulani la jadi. Kwa hivyo istilahi inamaanisha watu wa asili, wenyeji au jamii wahamaji, jamii nyingi zinazofanya kazi pamoja, au vikundi vingine, kadiri inavyofaa.

Header Photo: © Grazia Borrini-Feyerabend