Mambo ya Kujifunza katika Utetezi

Kama sehemu ya mchakato wa kujiimarisha, mtandao wa kitaifa wa Kongani la Kimataifa unapaswa kuzingatia kwa makini ni aina gani za sera za kimila, kisheria au nyinginezo na utambuzi na uungwaji mkono zinafaa katika muktadha wake. Ni muhimu sana kwamba jamii za wamiliki wa Kongani la Kimataifa zitetee aina mahususi ya utambuzi na uungwaji mkono baada ya uchunguzi wa kina na wa uwazi wa manufaa na hatari za machaguo mbalimbali yanayowezekana, na chini ya mamlaka na wajibu wa wawakilishi wao halali. Utambuzi ufaao na uungwaji mkono vinaweza kusaidia jamii kupata na kutekeleza haki zao za pamoja na wajibu kwa maeneo yao ya umiliki. Utambuzi na uungwaji mkono usiofaa na usiotosheleza, hata hivyo, unaweza kudhuru na kuleta ushawishi na athari zisizohitajika.

Jamii mbalimbali za wamiliki ambazo hutetea kwa pamoja zina nguvu na zina uwezekano mkubwa wa kupata kile wanachohitaji. Wanaweza pia kutaka kushirikisha washirika wengine. Harakati za kitaifa za haki za ardhi, haki za wakulima wadogo na haki za watu wa asili zinaweza kuwa washirika wenye nguvu za wamiliki wa jamuiya za maeneo yao ya hifadhi ya jadi zikishirikiana na mashirika ya kiraia za kuendeleza harakati za uhifadhi wa mazingira, uwepo wa vipato vya kujikimu endelevu na haki za binadamu kuhusu mazingira. Linapokuja suala la jinsi ya kujihusisha vyama vya siasa, kama chaguo la kuchukuliwa na kila mtandao wa Kongani la Kimataifa, lichukuliwe kwa umakini mkubwa.

Mwezeshaji anayefanya kazi na Mtandao wa Kongani la Kimataifa anaweza kusisitiza kwamba mipango ya utetezi iliyofaulu ina lengo lililo wazi na lililojengewa hoja vyema (k.m. marekebisho mahususi ya sera au ufadhili wa mpango mahususi) na inaungwa mkono na mifano thabiti, chanya, bajeti iliyokusudiwa na jamii ambayo ina umoja na pana iwezekanavyo. Muhimu zaidi, mwezeshaji anaweza pia kutengeneza mahusiano na mtu mmoja au wachache au mashirika yenye ujuzi wa kisheria.Kimsingi, utetezi wowote mahususi ungeungwa mkono na angalau asasi moja ya kiraia yenye ujuzi wa kisheria, yenye uwezo wa kutoa mikakati na ufumbuzi wa kisheria, kuwasilisha malalamiko, kufuatilia kesi mahususi, kusaidia katika masuala ya ardhi na rasilimali na migogoro, kuunga mkono utambuzi wa Kongani la Kimataifa maalum, kutoa ulinzi kwa haki za pamoja kila zinapopingwa, na kuwafunza wanajamii juu ya ujuzi wa wasaidizi wa kisheria. 

Note

Mtazamo wa utetezi utategemea muktadha, maono, na mahitaji ya wale wanaohusika. Tazama Kumbukumbu za Rasilimali kwa maelezo zaidi kuhusu:

Note

Hatimaye, manufaa makubwa zaidi ya utetezi wa pamoja ni uwezo wa kujenga umati mkubwa kwa ajili ya mabadiliko katika nchi yoyote ile. Wanachama na washirika wa Kongani la Kimataifa wamejifunza kwamba:

  • Mtu yeyote ana uwezo wa kuwa wakili; hakuna sababu ya jamii ya wamiliki kuogopa kutafuta utambuzi na kuungwa mkono kwa eneo lake, lakini kufanya hivyo na jamii nyingine na washirika ni msaada mkubwa.
  • Utetezi una nguvu zaidi wakati mitandao na washirika mbalimbali wanapendekeza mabadiliko ya sera yanayofanana na wakati mabadiliko kama hayo yana mvuto mpana kwa washirika wengi katika jamii.