Kiolezo cha Muungano wa Kongani la Kimataifa kwa ajili ya kuweka kumbukumbu za eneo la hifadhi ya jadi, na zana zingine muhimu

Zana mbili zifuatazo zinastahili kumulikwa haswa:

Kiolezo cha Muungano wa Kongani la Kimataifa cha kuhifadhia taarifa muhimu kuhusu eneo la hifadhi ya jadi

Pakua kiolezo katika Word (inakamilishwa kwa kutumia mtandao) au PDF (inakamilishwa kwa mkono wakati wa mjadala mashinani).

Kiolezo hiki siyo mbadala wa njia nyingine za uwekaji kumbukumbu, kama vile ramani, filamu, hadithi mbalimbali, na kadhalika, badala yake, huwa mahali rahisi pa kuhifadhi taarifa muhimu. Taarifa hii inaweza kuwa muhimu kwa madhumuni mengi ikiwa ni pamoja na kuandaa kumbukumbu kwa kanzidata za kitaifa au kimataifa ambazo jamii zinaweza kuchagua kujiunga (kwa mfano, Masijala ya Kitaifa ya Kongani la Kimataifa, kanzidata ya LandMark, Masijala ya Kimataifa ya Kongani la Kimataifa na Kanzidata ya Maeneo Yanayohifadhiwa Duniani, na kadhalika) na kuelezea eneo la hifadhi ya jadi kwa mipango mbalimbali. Kiolezo pia kinaweza kutumika kama dodoso kuongoza jamii moja au kadhaa kwa majadiliano ya mashinani.

Muhimu: Kiolezo kinaweza kujazwa na mshiriki mmoja au kadhaa wa timu ya uwezeshaji kwa kuzingatia matokeo ya mikutano na shughuli kadhaa. Kiolezo kilichokamilishwa kinapaswa kupatikana bure ili jamii ikifikie kwa urahisi, kukirejea na kutoa maoni.

Zana ya uchoraji ya Mapeo

Mapeo imetengenezwa mahususi na Demokrasia ya Kidijitali kwa madhumuni ya wenyeji kuhifadhi kumbukumbu za ushirikishwaji jamii za asili na wenyeji, kwa ushirikiano wa karibu na watu wa asili na mashirika wenyeji katika Amazon. Ni zana rahisi kutumia ambayo inafanya kazi vizuri katika simu za mkononi na kompyuta mpakato, bila kuwa na haja ya kuunganisha na intaneti, kuruhusu kutengeneza ramani ya eneo kwa kutumia alama za Mfumo wa Kijiografia unaonesha sehemu halisi katika uso wa ardhi, kuongeza picha na maelezo kupitia kiolesura rahisi. Takwimu zote zinasalia kikamilifu chini ya udhibiti wa jamii, ambapo wanaweza kuchagua kama watasambaza taarifa yao yoyote nje. Mapeo pia ina vipengele vya kuwezesha usajili katika Masijala ya Kimataifa ya Kongani la Kimataifa na Kanzidata ya Maeneo Yanayohifadhiwa Ulimwenguni.

 

 

 

 

Note

Kikundikazi cha Muungano wa Kongani la Kimataifa cha kuweka kumbukumbu ya maeneo ya hifadhi ya jadi kinalenga kutoa taarifa mpya na kuwezesha kubadilishana maarifa kuhusu zana, mbinu mbalimbali na rasilimali.