Vinjari baadhi ya maeneo ya hifadhi ya jadi

Neno ‘Maeneo ya hifadhi ya jadi ya Kongani la Kimataifa’ — humaanisha “maeneo yanayotawaliwa, kusimamiwa na kuhifadhiwa-kuhudumiwa na watu wa asili na jamii za wenyeji”. Hii inammanisha hali ya zamani, iliyoenea, tofauti na inayobadilika ambayo ina matukio na majina mengi tofauti ulimwenguni. Kwa wamilikiwamiliki wa “maeneo ya hifadhi ya jadi” kama haya, uhusiano kati ya jamii yao na maeneo ya hifadhi ya jadi ni mkubwa kuliko neno au kifungu chochote cha maneno kinaweza kuelezea. Ni dhamana ya kipato cha kujikimu, nishati na afya. Ni chanzo cha utambulisho na utamaduni, utawala binafsi na uhuru. Ni kiungo kati ya vizazi, kuhifadhi kumbukumbu za zamani na kuzifungamanisha na siku zijazo. Ni msingi ambao jamii hujifunza, kutambua tunu na kuendeleza mahusiano na kujitawala. Kwa wengi, pia ni uhusiano kati ya ukweli unaoonekana na usioonekana, mali na utajiri wa kiroho. Katika eneo na mazingira yapo maisha ya jamii na utu na kujiamini kama watu.