Kushughulikia mabadiliko katika ustahimilivu na usalama baada ya muda: Maswali ya kujadili mashinani

Nguvu, udhaifu, matishio na fursa za ustahimilivu na usalama (tazama #Kuelewa ) zina uwezekano wa kubadilika baada ya muda. Ili kusaidia kufuatilia mabadiliko haya, ni muhimu kutambua viashiria muhimu na kuvifuatilia baada ya muda. Kwa mfano, kama sehemu ya mijadala ya mashinani, jamii yako inaweza kutaka kubainisha angalau kiashirio kimoja cha maana kwa kila moja ya “nguzo tano” za eneo la hifadhi ya jadi salama na stahimilivu (ona #Chombo cha Ustahimilivu na Usalama). Nguzo hizo ni:

  • uadilifu na nguvu ya jamii ya wamiliki;
  • uhusiano wa karibu kati ya jamii na eneo lake;
  • utendajikazi wa taasisi ya utawala;
  • thali ya uhifadhi wa eneo; na
  • Kipato cha kujikimu na ustawi wa jamii.

Kwa kila mmoja, unaweza kuuliza:

  • Ni jambo gani, mali au thamani gani tunaweza kupima au kutathmini ambalo linaweza kutuambia kama hii ‘nguzo’ inabadilika kuwa bora (au mbaya zaidi)? 
  • Je, tunawezaje kupima au kutathmini hilo, kwa vitendo?
  • Nani angeweza kufanya hivyo? Je, kuna mtu yuko tayari kufuatilia mabadiliko? Wengine wanaweza kufanya nini ili kusaidia?
  • Ni kwa muda gani tutakutana tena ili kujadili mabadiliko?
Note

Unaweza kupakua hapa mifano ya viashiria vya ustahimilivu na usalama wa maeneo ya hifadhi ya jadi, ambavyo vilitengenezwa kwa ajili ya kutumiwa na jamii maalum za wamiliki. Kila jamii inapaswa kutengeneza viashiria vyake, vinavyoonyesha hali yake yenyewe: Viashiria vya ustahimilivu na usalama vya mfano vya Kongani la Kimataifa na kama pdf