2
Kuweka kumbukumbu za eneo la hifadhi ya jadi: Maswali ya kujadili mashinani
Maswali haya yanaweza kusaidia jamii kuamua jinsi ya kutengeneza kumbukumbu za ziada kuhusu eneo lake la hifadhi.
- Je, taarifa kuhusu eneo la hifadhi ya jadi zipo tayari na zinapatikana kwa urahisi kwa jamii yetu?
- Je, imesambazwa kwa uwazi na kujadiliwa?
- Ni miundombinu gani imetumika kuweka hiz taarifa muhimu – kwa mfano ramani, orodha, picha, hadithi, nyaraka…?
- Je, kuna miundombinu ambayo inaweza kuwa muhimu hasa kwa jamii yetu? Kwa mfano, taarifa ya mdomo inapaswa kuwa kumbukumbu kupitia ushirikishwaji wa watu wote kwa kutumia ramani au filamu?
- Je, kuna taarifa bado hazijapatikana/hazipo katika kumbukumbu na kwamba itakuwa muhimu kuwa nazo?
- Je, hizi kumbukumbu zinawezakupatikanaje /kuundwa/kutengenezwa?
- Je, jamii yetu itafanya nini na taarifa zilizopo katika kumbukumbu?
- Kumbukumbu zitasambazwa vipi na nani? (Angalia pia #Chukua hatua na kufanya mawasiliano na #Chukua hatua ukiwa na wengine)
- Je, kuna wasiwasi au hatari kutokana na kutengeneza au kusambaza kumbukumbuku? Je, tunawezaje kushughulikia hatari hizo?
- Je, kuna fursa mpya kutokana na kutengeneza au kusambaza kumbukumbu? Je, tunawezaje kuchukua hatua juu ya haya?