Kuadhimisha kujitoa kwa ajili ya eneo la hifadhi ya jadi: Maswali ya kujadili mashinani

Sherehe inaweza kuangazia kile ambacho jamii imepata na kile inachotaka kufanikiwa zaidi, kuzalisha fahari na nguvu mpya na kuonyesha wazi dhamira ya pamoja ya kuhifadhi eneo la hifadhi ya jadi. Sherehe ni muhimu ili kuweka kumbukumbu za pamoja, kujitambua na umoja katikati ya maisha ya jamii.

Tunatamani kusherehekea kitu gani na kwa nini?

  • Je, maono/dira yetu ya pamoja na kujitoa kwa eneo la hifadhi ya jadi kunapaswa kuainishwa na sherehe au tukio lingine na ushiriki wa jamii kwa ujumla?
  • Je, matokeo chanya ya sherehe hiyo yangekuwa yapi? Je, kutakuwa na matatizo yoyote yanayoweza kutokea kutokana na kufanya sherehe? Ikiwa kuna matatizo yanayoweza kutokea, tunaweza kufanya nini ili kukabiliana nayo?
  • Ni aina gani ya tukio lingefaa – kwa mfano, sherehe ya kitamaduni, ikiwezekana kujumuisha mambo ya kiroho? Tukio la ‘kisasa’ lenye hotuba na kuweka saini? Mchanganyiko wa mbinu? Tukio kubwa lenye vipengele mbalimbali (chakula na vinywaji, nyimbo, ngoma, maonyesho ya sanaa, maonesho ya bidhaa za asili kutoka eneo la hifadhi ya jadi, n.k.)?
  • Tutatumia maneno gani kurejea eneo letu la hifadhi ya jadi na jamii yetu ya wamiliki? Je, tunalo jina maalum la eneo ambalo tayari limejadiliwa na kukubaliwa kwa mapana na jamii kwa ujumla ambalo linaweza kuthibitishwa tena na kutumika kwa mapana/sehemu mbalimbali? (Angalia pia #Chukua hatua na kufanya mawasiliano)
  • Je, tutaandaaje sherehe ili kuhakikisha tunafikia matokeo yanayotarajiwa? Kwa mfano, tunapaswa kusambaza taarifa au kutoa tamko juu ya maono/dira yetu tunayoyatarajia? Je, tusambaze taarifa za kujitambua kwetu kama wamiliki, kwa mfano ahadi, mkataba au kanuni na vigezo tulivyokubaliana? Kama ni hivyo, nani inapaswa kutamka kauli hizo – kwa mfano wazee wa jamii, vijana, baraza linaloongoza la eneo la hifadhi ya jadi? Je, tunapaswa kujumuisha katika mpango mjadala wa hati yoyote rasmi inayotambua jamii yetu kama mmiliki wa eneo?

 

Tunapangaje sherehe?

  • Ikiwa tunafanya sherehe, inapaswa kufanywa lini? Je, inafaa kuendana na maonyesho ya soko au mapumziko? Je! tunasherehekea baada ya matembezi ya pamoja katika eneo, kama inavyofanywa katika mila nyingi za kitamaduni? Ikiwa ni hivyo, msimu na kipindi gani kitafaa vizuri zaidi?
  • Je, kila mtu katika jamii ashirikishwe? Wazee wanapaswa kutimiza wajibu gani? Vijana? Wanawake? Wanaume? Watoto?
  • Nani anafaa kualikwa kwenye sherehe (kwa mfano jamii yetu pekee au jamii nyinginezo, mamlaka ya jimbo/taifa, washirika, na kadhalika)?
  • Nani anafaa kusaidia (kwa mfano kwa muda, ufadhili, chakula, vinywaji, muziki au michango mingine)?
Note

Hakuna ‘wakati bora zaidi’:  Kusherehekea wakati wa matishio makubwa au fursa mpya inaweza kuthibitisha maono/dira ya jamii na kuchochea hamasa kuchukua hatua. Sherehe inayofanyika baada ya kutengeneza mpango madhubuti wa utekelezaji kufikia maono/dira ya pamoja ambayo yamekubaliwa yanaweza kuchochea utayari wa kushiriki na kuchukua hatua (tazama pia #Chukua hatua na Uwasiliane).