Chukua hatua ukiwa na Wengine

Jamii nyingi za wamiliki hukabiliana na changamoto zinazofanana. Jamii yako ina uwezekano wa kufaidika kwa kuwashirikisha uzoefu na kuunganisha nguvu na wengine. Kwa maana hii, kujiimarisha hatimaye kunahusisha kuimarishana kati ya wenzao na washirika, ambapo kwa ujumla huanza kutokana na aina fulani ya mtandao wa ushirikiano.

Kitaifa (na wakati mwingine kimataifa) kuunda mtandao na kupanga kwa ajili ya hatua shirikishiinaweza kusaidia kutengeneza idadi kubwa ya watu muhimu wa kuunga mkono maeneo ya hifadhi ya jadi, ambayo kwa upande hutoa:

  • ufahamu wa pande zote na mshikamano, ikijumuisha kushughulikia matishio kwa maeneo ya hifadhi ya jadi;
  • kuimarika kwa nyenzo za kuchukua hatua (zilizokusanywa pamoja kutoka kwa vyanzo vingi);
  • uelewa mzuri juu ya masuala na vipaumbele yanayowahusu wote, ikijumuisha kushughulikia fursa na kutumia vyema rasilimali;
  • kuboresha mwonekano wa kitaifa na kimataifa wa manufaa mapana ya maeneo ya hifadhi ya jadi; na
  • ufanisi katika utetezi wa sera na utendaji uliyoboreshwa

Juhudi za pamoja mara nyingi huanza kwa kubadilishana na kujifunza kati ya jamii za wamiliki jirani na washirika- kwa mfano ziara za mafunzo, midahalo, warsha, au msaada wa kutatua tatizo.

Baada ya muda, mitandao au majukwaa ya kawaida zaidi au hata rasmi yanaweza kubadilika na kuendeleza kusaidiana kwa vitendo na juhudi za utetezi. Mifano ni pamoja na:   

  • uchambuzi na mipango ya pamoja ili kutambua na kushughulikia masuala na vipaumbele vya kitaifa na kimataifa;
  • kampeni za mawasiliano ili kuongeza mwonekano wa maeneo ya hifadhi ya jadi na kutafuta msaada wa kushughulikia matishio mahususi na malengo mengine ya utetezi;
  • mchakato wa msaada na mapitio kwa wenzao, ikijumuisha yale muhimu kwa usajili kitaifa na kimataifa ya Kongani la Kimataifa na 
  • kampeni za utetezi kwa ajili ya kutambulika vyema na msaada, ikijumuisha kuboresha sheria na sera za kitaifa na/au kimataifa zinazoathiri maeneo ya hifadhi ya jadi.

Header Photo: © Bruno Manser Fund