Chukua hatua na Fanya mawasiliano

Kwa mchakato wa kujiimarisha wenyewe ili kutoa matokeo thabiti, hivi punde jamii yako itahitaji ‘kuchukua hatua’. Hii kwa kawaida inajumuisha kuendeleza na kutekeleza mpango mmoja au zaidi mahususi.

Juhudi hizi zinapaswa kutokana na uelewa na uwezo wa jamii yako juu ya changamoto na matishio na fursa inazokabiliana nazo (tazama #Fahamu) kuhusiana na jukumu lake kama mlezi na mbeba maono/dira yanayotarajiwa (tazama #Maono/dira na Sherehekea). Kwa maneno mengine, jamii yako inapaswa kuzingatia na kukubaliana juu ya kile kinachohitajika kutokea ili maono/dira yake ya pamoja ya eneo la hifadhi ya jadi yawe ya kweli/yatimie.


Kwa mfano, ikiwa jamii yako inataka kudumisha eneo lake kwa maisha yenye afya, inahitaji kuzuia uanzishwaji wa viwanda vinavyoharibu ikolojia. Hii inaweza kuhusisha kufikiria jinsi ya kuzuia viwanda kama hivyo kwa kupata makubaliano ya serikali. Ikiwa jamii inataka vijana wa eneo hilo kukaa hapo, badala ya kuhamia mijini, inaweza kuboresha elimu na fursa za kipato cha kujikimu na maisha. Hili linahitaji maono/dira, mipango ya kujitoa na rasilimali.

Kuhusiana na kutengeneza mipango ya utekelezaji, na kwa michakato ya kujiimarisha kwa upana zaidi, jamii yako kama mmiliki inaweza kuwa na uhusiano na wengine – kama vile jamii nyingine, mashirika washirika na serikali – na kuwasiliana kwa njia za kimkakati kuhusu eneo lake la jadi. Hii inaweza kutokea katika viwango mbalimbali – kwa mfano, mitaa, mazingira, kitaifa na kimataifa – na kwa sababu mbalimbali. Mipango ya mawasiliano mara nyingi hupangwa kuwajulisha wengine kuhusu eneo la hifadhi ya jadi na hatua za jamii na haki na wajibu wa kimila/kikanuni. Lengo moja la pamoja ni kuhakikisha kuwa jamii yako inatambulika ipasavyo, inaungwa mkono na kuheshimiwa, na nyingine ni kupata msaada katika shughuli maalum, kulingana na jinsi jamii ilivyoamua.

Note

faida nyingi za mawasiliano mazuri: Mipango ya mawasiliano mara nyingi huleta manufaa kwa jamii ambayo inakwenda zaidi ya yaliyo dhahiri. Kwa mfano, kupitia kuanzisha na kusambaza mawasiliano, jamii inaimarisha ufahamu wake wa ndani na uwazi, na hivyo, inaboresha utawala. Kuwasiliana pia hutengeneza uhusiano na jamii zingine. Unaweza kuhamasisha jamii zingine… na, vivyo hivyo, kusikia kutoka kwao, kugundua mfanano, kujifunza kutoka kwao na hatimaye kushirikiana nao (tazama #Chukua hatua na Wengine). Mbinu za mawasiliano zinahitaji kubuniwa kimkakati na kulengwa kulingana na muktadha na mahitaji mahususi. Taarifa muhimu na nyenzo kuna uwezekano zitakuwepo kutoka kwa #tafakari, #kumbukumbu na vipengele vya #kuelewa lakini zaidi inaweza kuzalishwa na Timu ya Mawasiliano ya jamii iliyojitoa, ambayo inapaswa hasa kuwa na weledi na iliyochangamka.



Header Photo: © Ashish Kothari