Weka dire & Sherehekea

Wakati muhimu sana wa mchakato wowote wa kujiimarisha ni wakati jamii inajitambua kama mhusika na mmiliki wa eneo lake la jadi na kujitoa kwa pamoja kudumisha jukumu hilo katika siku zijazo. Huku kujitoa kunaweza kuonekana tofauti kwa watu na jamii tofauti, lakini kwa kawaida hujikita kwenye mkusanyiko wa uwezo na utashi wa kutawala na kusimamia eneo husika.

Kujitambua kama mmiliki wa jamii mara nyingi huwa na nguvu zaidi inapojengwa juu ya au pamoja na maono/dira ya pamoja ya eneo la hifadhi ya jadi. Baadhi ya jamii huhisi kwamba maono/dira kama haya yamo katika imani zao za kiroho na jinsi wanavyoishi, lakini bado unaona kuwa ni muhimu kuifanya iwe wazi. Wengine wanaweza kuona ni muhimu kuzalisha, au kuendeleza zaidi, na kuyasanifu yale maono/dira. Ingawa kukubaliana juu ya maono/dira ya pamoja siyo rahisi, lengo hili mara nyingi linaweza kufanikiwa kwa uwezeshaji makini na muda wa kujadili na kutathmini machaguo mengine.

Wakati wa kujitambua kwa pamoja kwa jamii yako unaweza kufikia kilele katika tukio ambalo utaweza thibitisha maono/dira ya siku zijazo unayotaka, jitoa kwa jukumu lako kama wamiliki na uwashe shauku na hisia zako za umoja. Hii inaweza kuhitaji kiasi kikubwa cha maandalizi ya awali, kuendeleza vipengele vya uelewa wa pamoja ambayo inaweza kuchukua miezi au miaka kukua.

Katika hali zote, ikiwa na wakati jamii yako inajitambua kama mmiliki wa eneo la hifadhi ya jadi na inajitoa kuendelea na jukumu hilo… wakati unaitaka sherehe au tukio lingine linalofaa!




Header Photo: © Ashish Kothari