1
Unapanga kujiimarisha wenyewe? Maswali ya kujadili mashinani
Bila kujali hali ya eneo la hifadhi ya jadi, maswali haya yanaweza kukusaidia kupanga mchakato wako wa kujiimarisha:
- Je, ni nini matumaini na mashaka/wasiwasi ya jamii yetu kuhusu eneo letu la hifadhi ya jadi?
- Je, tunataka kushiriki katika uimarishaji wa eneo letu la hifadhi ya jadi?
- Nani ahusishwe katika kujadili na kuchukua hatua?
- Nani ataratibu, atawezesha, na atafuatilia mchakato?
- Vipi na namna gani, tunapaswa kukutana wakati wa mchakato?
- Tunapozingatia vipengele saba (tazama utangulizi) vya mchakato wa kujiimarisha wenyewe, vipi ni muhimu kwetu?
- Tutaanzia wapi, na lini?
- Je, tunazo rasilimali tunazohitaji kusaidia mchakato huu za kutosha? Ikiwa sivyo, zitapatikanaje?