Kutengeneza mtandao wa maeneo ya hifadhi ya jadi: Machaguo na maswali ya kujadili mashinani
Mtandao wa Kongani la Kimataifa ni mtandao wa watu binafsi, jamii na mashirika yaliyo tayari kushirikiana na kutoa ushauri na msaada kwa kila mmoja wao katika masuala mbalimbali kuhusu maeneo ya hifadhi ya jadi (kwa mfano, utendaji, sera, mienendo, matishio, fursa, rasilimali…).
…… baadhi ya machaguo ya mitandao ni pamoja na…
- Kikundi kazi – Huu ni mtandao usio rasmi ambapo wamiliki wa eneo la hifadhi ya jadi, mashirika washirika, na wanaharakati binafsi na wataalam hukusanyika mara kwa mara ili kubadilishana mawazo na kufanyia kazi masuala ya yanayowakabili wote.
- Muungano au jukwaa – Hii ni mitandao rasmi zaidi inayojitolea kwa lengo moja, hasa kushughulikia masuala mahususi, yanayoshinikiza—kwa mfano, muungano dhidi ya tishio lililo karibu la uporaji wa ardhi au jukwaa la kuunga mkono sera maalum ya kitaifa.
- Mtandao wa msaada na mapitio ya washirika walio katika ngazi moja miongoni mwa maeneo ya hifadhi ya jadi – Hizi ni mbinu zinazotolewa kusaidiana kwa hiari na kuhakikisha kuwa jamii za wamiliki zinaweka pamoja mawasilisho yenye maana kwa masijala kitaifa au kimataifa za maeneo ya hifadhi ya jadi. Mtandao unakubaliana na kanuni na taratibu za mawasilisho hayo ambazo zinaungwa mkono na kupitiwa na washirika walio katika ngazi moja.
- Muungano au shirikisho – Haya ni mashirika rasmi, kama vile chama au shirikisho ambalo linawakilisha maslahi ya pamoja miongoni mwa wamiliki wa maeneo ya hifadhi ya jadi. Tofauti na mingine, mtindo huu unaruhusu mtandao kupokea na kutumia rasilimali muhimu. Pia hutoa uwakilishi unaoaminika wakati wa kuchangamana na wengine, kama vile serikali za mikoa au kitaifa.
Bila kujali aina ya mtandao, ni muhimu litokee kwenye hitaji miongoni mwa jamii na hivyo likidhi hitaji hilo na changamoto na vipaumbele vya pamoja.
Ikiwa mtandao wa eneo la hifadhi ya jadi bado haupo katika eneo fulani au nchi, kuandaa mkutano kati ya wawakilishi wa wamiliki wa jamii wa maeneo ya hifadhi ya jadi ni njia yenye ufanisi kuanzia. The mkutano hutengeneza fursa kwa wamiliki kusikiliza mahitaji na mawazo ya kila mmoja na kuweka msimamo wa pamoja, mara nyingi kwa kuzingatia matishio na fursa za pamoja zinazotambulika. Kama ambavyo jamii za wamiliki na washirika wao hutambua mahitaji ya wote na shughuli za pamoja ili kukidhi mahitaji hayo, wanaweza kuamua kuendeleza aina fulani ya ushirikiano unaoendelea kama mtandao.
…maswali ya kuzingatia unaposhiriki katika mtandao
- Je, kuna mahitaji, changamoto au vipaumbele ambavyo tunaweza kushughulikia vyema kupitia mitandao na kwa pamoja kupanga na washirika walio katika ngazi moja na washirika? jamii yetu katika mtandao na wawakilishi hao wangetoaje mrejesho kwa jamii?
- Je, jamii yetu imewahi kushiriki katika uhamasishaji? Tumejifunza nini katika mchakato huo?
- Je, jamii yetu inazo rasilimali kwa ajili na kutengeneza mtandao na maandalizi ya pamoja?
- Je, kuna hali maalum au mazingira ambayo yanahitaji kuwepo ili jamii yetu ishiriki katika mtandao au shughuli ya pamoja ya kuandaa?
- Je, jamii yetu inawafahamu wenzao na washirika tunaofikiria kujiunga nao katika mtandao? Hapo awali tumewahi kuwashirikisha taarifa, uchambuzi wa hali na mipango yetu, au kushiriki katika tukio pamoja nao? Ikiwa sivyo, tunaweza kujaribu hilo, kabla sisi hatujaingia katika jambo ambalo litatushughulisha zaidi?
- Kama tukiamua kuunda au kujiunga na mtandao, nani angewakilisha jamii yetu kwenye mtandao na wawakilishi hao wangetoa vipi mrejesho kwa jamii?
Baadhi ya mitandao inaweza kubadilika na si rasmi. Mingine ni rasmi na imeundwa kwa uangalifu kwa ajili ya muktadha maalum au kushughulikia suala maalum. Mitandao yote inapaswa kuwa na uwezo wa kuwanufaisha wanachama wao binafsi, lakini mingi inaweza kufikia malengo mapana. Vipaumbele vya wanachama, muktadha wao, na rasilimali na uwezo wao vyote vinaweza kusaidia kufahamisha ni mbinu ipi ya mtandao inafaa zaidi.