Kuwa na maono/dira ya mustakabali unaotarajiwa wa eneo la hifadhi ya jadi: Maswali ya kujadili mashinani

Kuanzisha maono/dira ya pamoja ya mustakabali unaotarajiwa wa eneo la hifadhi ya jadi na jamuiya yake ya wamiliki, maswali yafuatayo yanaweza kuwa mwanzo mzuri:

  • Eneo letu la hifadhi ya jadi lingekuwaje ikiwa lingesitawi kikamilifu leo (‘bora zaidi kadiri linavyoweza kuwa lingeweza’)? Wacha tufikirie kwa muonekano (kwa mfano mazingira, asili, makazi ya watu, barabara, uwepo wa jamii, tabia dhahiri ya watu…) lakini pia sifa za ndani (kwa mfano ubora wa udongo, maji, hewa, ubora wa mifumo ya ikolojia, uwepo wa bioanuwai na tamaduni mbalimbali, hali ya ustawi…)
  • Eneo letu lingeonekanaje katika siku zijazo – kwa mfano miaka mitano, kumi, na hamsini kutoka sasa—kama ingewezekana kustawi kikamilifu? Tena, wacha tuifikirie kulingana na muonekano na sifa za ndani.

Washiriki mbalimbali katika mjadala wa mashinani wanaweza kuelezea mustakabali wao wanaotaka kwa eneo la hifadhi ya jadi kwa njia tofauti. Ikiwa ndivyo, timu ya uwezeshaji inaweza kufanya uchunguzi:

  • Je, kuna vipengele vinavyolingana miongoni mwa maono/dira yetu binafsi?
  • Je, tunaweza kuzitambua hizo na kukubaliana juu ya seti za vipengele vya msingi vya maono/dira ambayo sote tunashiriki?
  • Kulingana na maono/dira kama haya, je, tunaweza kuthibitisha tena jukumu letu kama wamiliki?
Note

Timu ya uwezeshaji inaweza kutaka kuorodhesha vipengele vinavyolingana vya maono/dira ya pamoja na kuthibitisha kwamba kila mtu anakubaliana navyo.