‘Eneo la hifadhi ya jadi’? Maswali ya kujadili mashinani

Kama sehemu ya mjadala mashinani, haya maswali yanaweza kutumika kusaidia jamii yako kutambua kama ndiyo mmilikimmiliki, mahusiani yao nae neo hilieneo la hifadhi ya jadi’ na, ikiwa ndivyo, eneo hilo liko katika hadhi gani.

…..muunganiko kati ya jamii na eneo lake la hifadhi

  • Je, jamii yetu ina ‘eneo’ maalum (eneo, makazi ya aina za viumbe) ambayo inahisi
  • Je, kuna muunganiko/mahusiano kati ya jamii yetu na eneo hili?
  • Ikiwa kuna muunganiko/mahusiano thabiti, je, inahusiana na (miongoni mwa uwezekano mwingine):
    • Maisha na kipato cha jamii yetu?
    • Hali ya usalama ya jamii yetu na uwezo wa kustahimili vikwazo
    • Historia ya jamii yetu, lugha, hali ya kiroho na/au utamaduni – hisia zetu za ‘sisi ni nani’?
    • Viumbe wengine wanaoishi katika eneo hilo – wanyama, mimea, mababu, mizimu, milima, mito?

…utawala wa jamii

  • Je, kuna maamuzi muhimu ambayo jamii yetu imechukua, na inaendelea kuchukua, kuhusu eneo letu?
  • Je, jamii yetu ina njia za kufanya maamuzi kuhusu eneo letu – kwa mfano kupitia mkutano mkuu, baraza la wazee, walimu wa kiroho, kamati, au viongozi wanaoaminika?
  • Je, jamii yetu ina kanuni kuhusu upatikanaji na matumizi ya eneo na rasilimali zake?
  • Je, tunaweza kutekeleza na kusimamia maamuzi na kanuni kuhusu eneo letu?

…matokeo chanya kwa mazingira na kipato cha kujikimu na ustawi wa jamii

  • Je, eneo letu limehifadhiwa vizuri? (Kwa mfano, mambo makubwa kuhusu mazingira yenye afya – kama vile rutuba ya udongo, ubora na kiasi cha maji, idadi ya spishi/aina za viumbe na mimea, uzalishaji katika kilimo, misitu na mimea, nk – kuwa inatunzwa au kuimarika?)
  • Je, kipato cha kujikimu na ustawi wa jamii ni endelevu na vinatoshelezwa na eneo? Kwa njia zipi?

Kwa ujumla: hali ya sasa ya eneo la hifadhi ya jadi

  • Je, eneo letu linabeba sifa tatu kuu za ‘eneo la hifadhi ya jadi’?
  • Ikiwa mojawapo ya sifa kuu hizi haina nguvu leo, je! Ni nini kimebadilika tangu wakati huo?
  • Je, eneo letu la hifadhi ya jadi limekamilika vizuri, limevurugwa, au tunalitamani liwe?
  • Ikiwa bado (au halipo tena) halijakamilika, je, tunataka kubadilisha hili, na je, tunaamini kwamba tunaweza?
Note

Katika kujadili hali halisi ya eneo la hifadhi ya jadi, kumbuka kuwa haya ni maamuzi yanayotokana na ukweli halisi, sio sifa za kupewa. Eneo la hifadhi ya jadi linaweza ‘kuvurugika’ kwa sababu nyingi. Labda jamii ilitawala eneo la hilo kwa muda mrefu lakini hivi sasa haiwezi tena kwa sababu ya migogoro au mashinikizo ya ndani au nje. Labda jamii inajali eneo la hifadhi ya jadi lakini haina nafasi kubwa au inayotambulika katika kufanya maamuzi. Labda mabadiliko ya tabianchi yanasumbua ufanisi wa juhudi za jamii na muda zaidi unahitajika kubadilika/kuendana nayo.