Fahamu

Mara taarifa ya kutosha kuhusu eneo la hifadhi ya jadi inapokusanywa na kusambazwa ndani ya jamii yako (tazama #Kumbukumbu), kujiimarisha kunaweza kuzingatia uelewa wa jamii kuhusu hali ya jumla au “afya” ya eneo la hifadhi ya jadi. Hasa, kwenye viungo vilivyo hapa chini, unaweza kupata zana rahisi na maswali ya kujadili mashinani kuelewa:

  • ustahimilivu na usalama wa eneo lako la hifadhi ya jadi;
  • uthabiti, changamoto, fursa na matishio vinavyokabili eneo lako la hifadhi ya jadi;
  • utawala wa eneo lako la hifadhi ya jadi; na
  • usimamizi wa eneo lako la hifadhi ya jadi.

Wakati mwongozo huu unaangazia eneo la hifadhi ya jadi, kipengele hiki kinashabihianishwa na uchanganuzi wa hali kwa mapana ambapo kwa kawaida hufanyika katika mchakato shirikishi katika ngazi ya jamii. Kama ambavyo nyanja za kiikolojia, kijamii, kitamaduni, kiroho, kisiasa na kiuchumi zinahusiana kiasili katika eneo la hifadhi ya jadi, jamii pia itajijadili yenyewe, ukweli wake na mustakabali wake.


Header Photo: © CENESTA