Panga na chukua hatua: Maswali ya kujadili mashinani 

Maswali hapa chini yanaweza kusaidia jamii yako katika kutengeneza picha rahisi ya uchanganuzi wa hali halisi ya eneo na kubaini vipaumbele kuelekea maono/dira ya mustakabali unaotarajiwa kwa eneo la hifadhi ya jadi na jamii ya wamiliki.

  • Kutafakari juu ya uwezo, changamoto, matishio, na fursa zinazokabili eneo letu la hifadhi ya jadi (ona #Elewa) na jukumu letu kama wamiliki (ona #Maono/dira na Kusherehekea), kile kinachopaswa kutokeaau kubadilisha, ili kufikia maono/dira chanya ya jamii yetu na eneo letu la hifadhi ya jadi, sasa na katika siku zijazo?
  • Je, kuna kitu kinachozuia mabadiliko hayo? Kama ndiyo, tunaweza kufanya nini ili kushinda au kupinga?

Je, ni zipi hatua zetu za kipaumbele?

Uwezekano ni pamoja na:

Kulinda eneo la hifadhi ya jadi dhidi ya matishio maalum

  • Kuimarisha kutambuliwa (kwa mfano kutambuliwa kikanuni) kwa umiliki wa jamii yetu au haki zingine.
  • Kuimarisha heshima ya utawala wetu wa jamii – nje na/au ndani
  • Kurejesha au kulinda vyema mifumo ikolojia au spishi katika eneo letu la hifadhi ya jadi
  • Kuimarisha uwezo wa eneo letu ili kusaidia kipato cha kujikimu kwa jamii yetu (kwa mfano kwa kutupatia maji, rasilimali za uzalishaji, ulinzi dhidi ya majanga)
  • Kuimarisha uhusiano kati ya eneo letu na jamii
  • Kupokea uungwaji mkono madhubuti wa kanuni za ndani kutoka kwa polisi, mashirika ya kitaalam, mfumo wa haki……
  • Kupata msaada bora wa kijamii na kiuchumi kutoka nje au ndani kufanya kile tunachohitaji kama wamiliki

Baada ya jamii yako kubainisha kipaumbele kimoja au zaidi cha kuchukua hatua, mipango madhubuti inaweza kuanza. Maswali ya majadiliano ni pamoja na:

…..Nini?, Nani? Na Lini? ya mpango kazi

  • Kwa kila mojawapo ya vipaumbele vyetu tulivyochagua, ni nini hasa tunachotaka kufanikisha?
  • Nani anaweza kuhusishwa?
    • Je, tunaweza kufanya nini kama jamii peke yetu? Je, kuna mabadiliko yoyote makubwa yanahitajika katika namna ambayo sisi wenyewe tunaishi, kufanya kazi na kujipanga?
    • Ni nani, ndani ya jamii yetu, anaweza (au angeweza) kutoa uongozi na msukumo?
    • Je, tunaona jukumu lolote maalum kwa wazee katika jamii yetu? Vijana? Wanawake? Wanaume? Watoto?
    • Nani mwingine ana (au ataweza) kuhusishwa na ajitoe kwa moyo?
    • Je, tunaweza kufanya nini kwa pamoja na jamii nyingine za wamiliki na washirika wa ndani?
    • Je, ni ushirikiano au miungano gani tunaweza kutegemea au kutafuta upya? (Ona pia #Chukua hatua na Wengine)
  • Ni ‘vipaumbele’ gani tunapaswa kuchukua?
  • Je, vipengele vya #mawasiliano vitahusika katika vipaumbele vyetu?
  • Tutachukua hatua lini? Ikiwezekana, je, tutawasiliana kabla (‘kutangaza tutakachofanya’) au baada ya tendo letu (‘kuripoti tulichokifanya’)?
  • Je, ni rasilimali gani za watu, fedha na nyinginezo tunazohitaji?
    • Je, tunazo nyenzo za kutekeleza vipaumbele vyetu – ikiwa ni pamoja na maarifa, ujuzi, taarifa, wakati, na teknolojia yoyote inayofaa (kwa mfano, kamera, Mfumo wa Kijiografia wa Kuonesha sehemu halisi, magari, vifaa vya mawasiliano…)?
    • Ni rasilimali zipi za ziada za kitaalam, watu na/au fedha tunazohitaji
    • Tunawezaje kupata rasilimali hizo za ziada – kwa mfano kutoka kwa jamii nyingine, washirika, wafadhili, na kadhalika?
    • Je, tutafuatilia na kuripoti vipi maendeleo yetu? (Angalia pia #Kagua & Upya).