Kumbukumbu
Kila eneo ni la kipekee na lenye vitu vingi… kuweka kumbukumbu zake vizuri kunaweza kuhisiwa kama kazi kubwa. Lakini unaweza kuanza kidogo kidogo na kuweka kumbukumbu taratibu, ukizingatia vipengele ambavyo ni muhimu zaidi kwa jamii yako katika eneo hilo kwa kuanza na taarifa ambazo tayari zinajulikana.
Kumbukumbu zilizoainishwa na jamii kuhusu eneo la hifadhi ya jadi zinaweza kutumika ndani ya jamii na kusaidia muunganiko wa nje. Inasaidia kuvipa nguvu ‘vipengele’ vingine vya kujiimarisha, ikiwa ni pamoja na kuweza kuwasiliana, kuona jinsi hali inavyobadilika na wakati, na hata kulinda eneo dhidi ya madhara.
Miundo muhimu ya uhifadhi wa kumbukumbu ni pamoja na picha, orodha, ramani, filamu, sanaa, rekodi za muziki, hadithi, mahojiano, na mengine mengi.
‘Maelezo’ tu huwa kumbukumbu wakati taarifa inawekwa katika muundo na kupangwa kwa njia zinazoifanya ipatikane kwa urahisi kwa rejea na matumizi ya baadaye. ‘Kumbukumbu nzuri’ hukamilika kwa kueleza kwa uwazi vipengele muhimu vya eneo na jamii, na jinsi maamuzi yanavyofanyika.
Kumbukumbu zote za eneo la hifadhi ya jadihifadhi zinapaswa kukusanywa, kusambazwa na kutumiwa kwa njia ambazo zitaamuliwa na jamii inayomiliki na kuheshimu haki zao, ikiwa ni pamoja na uamuzi huru na wa hiari.
Header Photo: © KESAN