Tazama jinsi wengine wanavyofanya!

Kutengeneza na kujitoa kwa ajili ya dira ya Hifadhi ya Amani Salween

Kholo Tamutaku Karer (kwa Kiingereza: Salween Peace Park) inachukua eneo la kilomita 5,485 za bonde la Mto Salween nchini Burma/Myanmar ambayo ni ya umuhimu mkubwa kwa viumbe hai duniani na kipato cha kujikimu kwa jamii nyingi za kiasili za Karen. Bonde la Mto Salween limekuwa eneo la hifadhi ya jadi la wamiliki wake wa kiasili wa Karen kwa takriban miaka elfu tatu, lakini kujitangaza kwa Hifadhi ya Amani ya Salween ni hivi karibuni (Desemba 2018).

Takriban wakazi 60,000 walipitia mchakato mrefu na mgumu wa mashauriano mfululizo, walitengeneza Mkataba pamoja na kanuni zilizokubaliwa, na mwishowe wakatangaza kwamba eneo lao limejitolea kutimiza matamanio yao makuu matatu: 1. amani na kujitawala; 2. uadilifu wa kimazingira; na 3. kudumisha utamaduni. Katika eneo ambalo limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe zaidi ya miaka 60, eneo hilo sasa limejitoa kuleta amani na kulinda ngome kubwa ya bioanuwai na utamaduni wa Karen (ikiwa ni pamoja na utawala wa kimila wa ardhi na mifumo ya usimamizi) kutoka kwa matishio ya zamani na mapya.



Photos: © Jittrapon Kaicome