Kuhusu mwongozo huu: uandishi na shukurani

Mwongozo huu unatokana na uzoefu katika maeneo husika wa Wanachama na Wanachama wa Heshima wa Muungano wa Kongani la Kimataifa la maeneo yanayohifadhiwa na jamii. Chapisho la awali lilitolewa na Muungano wa Kongani la Kimataifa la maeneo yanayohifadhiwa na jamii katika lugha tatu na kusambazwa mwaka wa 2017 (linapatikana kama faili la data la kudumu hapa). Toleo hili la sasa limejumuisha maoni na ya kujifunza tangu wakati huo. Inapaswa kurejewa kama:

Borrini-Feyerabend, G., J. Campese, na T. Niederberger (eds). 2021. Kuimarisha eneo lako la hifadhi ya jadi: mwongozo kutoka kwa jamii kwa ajili ya jamii. Toleo la mtandaoni: ssprocess.iccaconsortium.org Muungano wa Kongani la Kimataifa la maeneo yanayohifadhiwa na jamii.

Maoni na mapendekezo yako yanakaribishwa sana! Tafadhali yatume kwa  documenting@iccaconsortium.org na gbffilter@gmail.com.

Wahariri wangependa kuwashukuru wafanyakazi wenzao wengi katika Muungano wa Kongasni la Kimataifa la maeneo yanayohifadhiwa na jamii ambao walitoa taarifa na ushauri kwa ukarimu katika kuendeleza kazi hii. Wanawashukuru sana Carolina Amaya, Ghanimat Azhdari, Albert Chan Dzul, Christian Chatelain, Colleen Corrigan, Emma Courtine, Sergio Couto, Tiphaine Dalmas, Dave de Vera, Singay Dorji, Cristina Eghenter, Taghi M. Farvar, Marc Foggin, Delfin Ganapin , Felipe Gomez, Hugh Govan, Terence Hay-Edie, Jeremy Ironside, Joseph Itongwa, Sudeep Jana Thing, Holly Jonas, Alexis Kaboré, Bassima Katib, Ashish Kothari, Emma Lee, Paola Maldonado Tobar, Carmen Miranda Larrea, Briana Okuno, Casper Palmano , Neema Pathak Broome, Femy Pinto, Aili Pyhälä, Lucas Quintupuray, Jailab Rai, Ali Razmkhah, Vololona Rasoarimanana, Vanessa Reid, Salatou Sambou, Sutej Hugu, Marc Tognotti, Paul Sein Twa, Makko Sinandei, Aman Singh, Emmanuel Tabanao, Glai , Zelealem Tefera Ashenafi, Ehhteeh Wah, Kasmita Widodo na Yingyi Zhang.

Muundo wa picha: Eric Irungu na Ines Hirata

Muundo wa wavuti: Rashida Z. Suleiman na Jake McMurchie

Tafsiri: Jumapili Chenga

Uhariri: Cassian Sianga

Uratibu wa tafsiri kwa Kiswahili: Emmanuel Sulle na Gaëlle Le Gauyer

Shukrani: Mwongozo huu na kazi inayohusiana nazo ambazo umetokana nazo ulifadhiliwa kupitia Mpango wa Msaada wa Kimataifa kwa Maeneo yanayohifadhiwa na jamii, Mfuko wa Christensen na Shirika la Misaada la Uswidi kupitia SwedBio katika Kituo cha Ustahimilivu cha Stockholm. Muungano wa Kongani la Kimataifa la maeneo yanayohifadhiwa na jamii unawashukuru kwa moyo mkunjufu washirika hawa wa ufadhili ambao msaada wao wa kuaminika umekuwa wa muhimu katika kukamilisha kazi hii.

Kongani la Kimataifa la maeneo yanayohifadhiwa na jamii-Mpango wa Msaada wa Kimataifa kwa Kongani la Kimataifa la maeneo yanayohifadhiwa na jamii ni mpango wa ushirikiano unaotolewa wa Ruzuku Ndogondogo wa Kituo cha Mazingira Duniani unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na kufadhiliwa na Serikali ya Ujerumani, kupitia Wizara yake ya Shirikisho ya Mazingira, Uhifadhi wa Mazingira na Usalama wa Nyuklia. Washirika wakuu ni pamoja na Kituo cha Ufuatiliaji wa Uhifadhi wa Mazingira cha Umoja wa Mataifa, Mpango wa Kimataifa wa Hifadhi wa Shirika la Umoja wa Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira, Muungano wa Kongani la Kimataifa la maeneo yanayohifadhiwa na jamii na Sekretarieti ya Mkataba kuhusu Bioanuwai.

Hakimiliki: Creative Commons (CC BY-NC-SA), Muungano wa Kongani la Kimataifa la maeneo yanayohifadhiwa na jamii la mwaka 2021

Kudurufu uchapishaji wa chapisho hili kwa madhumuni ya kielimu au mengine yasiyo ya kibiashara umeidhinishwa bila kibali cha maandishi kutoka kwa mwenye hakimiliki ilihali chanzo kimekubaliwa kikamilifu. Kidurufu uchapishaji wa chapisho hili kwa ajili ya kuuza au madhumuni mengine ya kibiashara hairuhusiwi bila kibali cha maandishi kutoka kwa mwenye hakimiliki.
Header Photo © Pierluigi Ferrari